Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita vyawakwamisha ndani maelfu Ivory Coast :OCHA

Vita vyawakwamisha ndani maelfu Ivory Coast :OCHA

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa anasema kuwa hali ya raia kwenye mji wa Abidjan ni mbaya.

Pande zinazopigana kwa sasa zinatumia silaha nzito kushambulia maeneo waliko raia . Inaripotiwa kuwa mamia ya raia waliuawa kwenye visa viwili tofauti na wengine katika mapigano ya kawaida. Hata hivyo idadi kamili ya waliouawa bado haijulikani.

Kulingana na msemaji wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA Elizabeth Byrs ni kuwa kumeshuhudiwa mashambulizi dhidi ya ngome za Laurent Gbagbo huku kukisikia milipuko mikubwa kutoka kila mahali mjini Abidjan.

Hali kwenye mji huo imebaki kuwa tete huku mahospitali na magari ya kusafirisha wagonjwa yakiwa hayafanyi kazi kufuatia kuwepo kwa ukosefu wa usalama.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)