Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majadiliano yanafanyika baina ya UNOCI na wafuasi wa Gbagbo kusitisha vita Ivory Coast

Majadiliano yanafanyika baina ya UNOCI na wafuasi wa Gbagbo kusitisha vita Ivory Coast

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast UNOCI kinasema kuwa kimepata simu kutoka kwa maafisa wa ngazi za juu wanaoumuunga mkono Laurent Gbabo zinazosema kuwa amri imetolewa kwa vikosi vinavyomuunga mkono Gbagbo kuacha kupigana.

Kati ya waliopiga simu ni pamoja na jenerali Philippe Mangou aliye mkuu wa majeshi na makamanda Thiape Ksarat pamoja na jenerali Bruno Dogbo. UNOCI imeamrisha vikosi vyake kupokea silaha zao na kuwapa ulinzi wanajeshi wanaomuunga mkono Gbagbo.

Kwa mujibu wa UNOCI hivi sasa majadiliano yanaendelea kuhusu majeshi ya Gbagbo kuweka silaha chini na uwezekano wa kuondoka nchini kwa Rais Laurent Gbagbo. Hamadoun Toure ni kutoka UNOCI mjini Abdjan

(SAUTI YA HAMADOUN TOURE)