Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yapongezwa kwa jitihada zake za kupambana na ukimwi:UM

Tanzania yapongezwa kwa jitihada zake za kupambana na ukimwi:UM

Serikali ya Tanzania leo mjini Dar es salaam imepongezwa kwa jitihada inazofanya katika vita dhidi ya ukimwi.

Akiwa ziarani nchini humo naibu Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro na mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS Michel Sidibe wamesema nchi za Afrika lazima zihakikishe zinafikia sufuri tatu, ikiwa ni pamoja na Sufuri kwa maambukizi mapya na sufuri kwa maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Migiro ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa Tanzania kupambana na ukimwi uliofanyika mjini Dar es salaam. Mwandishi wetu George Njogopa alikuwepo na kuandaa taarifa hii.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)