Skip to main content

Ban asikitishwa na ukandamizaji waandamanaji Syria

Ban asikitishwa na ukandamizaji waandamanaji Syria

Huku hali ya mambo ikiendelea kuchacha nchini Syria ambako watu kadhaa wameripotiwa kupoteza maisha wakati waliposhambuliwa kwenye maandamano, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani hatua ya utumiaji nguvu dhidi ya raia.

Taarifa kutoka nchini humo zinasema watu kadhaa wamearifiwa kufariki dunia kutokana na kushambuliwa na vikosi vya serikali vinavyojaribu kudhibiti maandamano ya amani.

Akizungumzia hali hiyo, Ban ametaka kukomeshwa mara moja utumiaji wa nguvu ili kudhibiti maandamano ya raia na akaitaka serikali ya Syria kuhakikisha inaheshimu na kuzingatia sheria za kimataifa.

Ameihimiza serikali ya nchi hiyo kuzingatia vipaumbele vinavyohimizwa na wananchi ambao wanataka kufanyika kwa  mageuzi kwenye mifumo yote ya kiutendaji.