Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aipongeza Kenya kwa kuendeleza nishati safi na salama

Ban aipongeza Kenya kwa kuendeleza nishati safi na salama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa amefurahishwa na kushangazwa na namna Kenya inavyoweza kukusanya miale inayotoka kwenye volcano itokayo kwenye bonde la ufa na kuzalisha nishati ya umeme.

Akizungumza mwishoni mwa wiki mjini Nairobi, Ban amesifu hatua hiyo akisema inaweza kuwa mkombozi mkubwa wa upatikanaji wa nishati ya uhakika na kupunguza kiwango cha uzalishaji wa hewa chafu ya carbon angani.

Katibu Mkuu huyo amesema hayo baada ya kutembelea mtambo wa Olkaria ulioko karibu na mji wa Naivasha ambako alisisitiza kuwa ugunduzi wa namna hiyo ni suluhisho la pekee la kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Amesema Umoja wa Mataifa, Benki ya Dunia pamoja na wahisani wengine wa maendeleo wako tayari kuunga mkono miradi ya namna hiyo ambayo inatoa mchango mkubwa kwa maendeleo endelevu.