Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waliomuua mwandishi Iraq wachukuliwe hatua:UNESCO

Waliomuua mwandishi Iraq wachukuliwe hatua:UNESCO

Mkuu wa shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova amelaani mauaji ya mwandishi wa habari raia wa Iraq akisema kuwa mauaji hayo ni lazima yachunguzwe.

Sabab al-Bazee ambaye alikuwa akifanyia kazi vitua kadha ni mmoja wa watu 20 waliouawa machi 29 wakati watu waliokuwa wamejihami walipovamia jengo moja la serikali kwenye mji wa Tikrit. Kifo cha bwana al-Bazee kinajiri baada ya mauaji ya mwandishi mwingine Hilal al-Ahmadi mwezi Februari mwaka huu.

Mwandishi huyo alikuwa mwandishi wa majarida yanayozungumzia ufisadi nchini Iraq ambaye alipigwa risasi alipokuwa akielekea kwenye mji wa kaskazini wa Mosul. Bokova ameutaka utawala nchini Iraq kufanya kila uwezalo kuwafikisha wahusika mbele ya sheriia