Skip to main content

Ban na Rais wa Iran wajadili hali Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Ban na Rais wa Iran wajadili hali Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza kwa njia ya simu jana Jumapili na Rais wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Mahmoud Ahmadinejad.

Wamejadili hali inayokabilia Afrika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati hivi sasa na hasa Libya, Bahrain na Yemen. Ban amesema amezitaka pande zote zinazohusika kwenye machafuko kujizuia na kuwalinda raia na amerejea wito wake kwa Libya kusitisha mapigano mara moja na kuruhusu wafanyakazi wa misaada kutekeleza wajibu wao.

Ban pia amemwezela Rais Ahmadinejad kuwa mwakilishi wake maalumu nchini libya Abdelilah al-Khatibu anashirikiana kwa karibu na jumuiya ya kimataifa, ikiwemo jumuiya ya nchi za Kiarabu na Muungano wa Afrika.

Naye naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro akizungumza mjini Dar es salaam Tanzania kuhusu juhudi za Umoja wa Mataifa katika hali ya Libya amesema:

(SAUTI YA ASHA ROSE MIGIRO)