Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Migiro ashiriki uzinduzi wa mkakati wa Ukimwi Tanzania

Migiro ashiriki uzinduzi wa mkakati wa Ukimwi Tanzania

Serikali ya Tanzania leo imezindua mkakati wa Kitaifa wa kinga ya ukimwi na mpango kazi kuhusu jinsia na ukimwi.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro aliyeko ziarani Tanzania kwa siku mbili.

Katika ziara hiyo Migiro ameambatana na mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Ukimwi UNAIDS Michel Sidibe na lengo lao kubwa ni kuongeza hamasa kwa nchi za Afrika kutilia mkazo kinga ili kupunguza maambukizi ya HIV na kufikia sufuri hasa kwa kizazi kipya. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)