Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya wakimbizi wa Somalia Kenya hairidhishi:UM

Hali ya wakimbizi wa Somalia Kenya hairidhishi:UM

Wakuu wa mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa wametoa taarifa kuelezea hofu yao kuhusu hali ya maisha ya wakimbizi zaidi ya 314,000 wa Kisomali walipozuru kambi ya Dadaab Kaskazini mashariki mwa Kenya.

Idadi ya wakimbizi inazidi kuongezeka kila siku na kusababisha msongamano mkubwa kwenye kambi hiyo ambayo ni kubwa kabisa ya wakimbizi duniani.

Wakuu hao Antonio Guterres wa UNHCR, Jossete Sheeran wa WFP na Michel Bachelet wa UN-Women wamesema ukame na miongo miwili ya vita imewalazimisha Wasomali kukimbia nchi yao na kupata hifadhi katika kambi tatu za Dadaab ambazo awali zilijengwa kuhifadhi wakimbizi wasio zidi 90,000. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)