Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndege ya UM yaanguka Kinshasa na kuuwa zaidi ya 10

Ndege ya UM yaanguka Kinshasa na kuuwa zaidi ya 10

Taarifa kutoka Jamhuri ya Kidekrasia ya Congo zinasema ndege ya mpango wa Umoja wa Mataifa MONUSCO imeanguka kwenye uwanja wa ndege wa Kinshasa na kuuwa watu takriban 10.

Kwa mujibu wa duru za habari za Umoja wa Mataifa ndege hiyo ilianguka ilipata ajali ilipoingia katika njia yake wakati rubani akijaribu kutua wakati kukiwa na mvua kubwa inanyesha mapema leo. Kwa mujibu wa walioshuhudia ndege hiyo ilikatika mapande mawili na kushika moto , watu wengine 16 wamearifiwa kujeruhiwa katika ajali hiyo.

Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Kisangani Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Mpango wa Umoja wa Mataifa MONUSCO ambao awali ulijulikana kama MONUC umekuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu mwaka 1999 na unatarajiwa kumaliza muda wake mwezi Juni mwaka huu.