Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya 300 wafa kwenye machafuko Duekoue:UM

Watu zaidi ya 300 wafa kwenye machafuko Duekoue:UM

Mapigano makali yamearifiwa katika mji mkuu wa wa Ivory Coast Abidjan baina ya wafuasi wanaomuunga mkono Alassane Ouattara anayetambukila kimataifa kama Rais na Laurent Gbagbo aliyegoma kuondoka madarakani.

Kwa mujibu wa duru za Umoja wa Mataifa na vyombo vingine vya habari, watu zaidi ya 330 wameuawa kwenye mji wa Magharibi wa Duekoue huku duru zingine zikisema idadi ya waliokuwa inafikia 1000.  Wafuasi wa Ouattara wanashikilia mji mkuu Yamossoukro, Duekoue na wanapambana ili kuchukua udhibiti wa Abidjan.

Naibu mkuu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Ivan Somonovic amewasili jana mjini Abidjan ili kutathimini hali ya haki za binadamu. Baada ya kuwasili ameelezea hofu yake juu ya kuzorota kwa hali , taarifa za mauaji ya halaiki na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu.

Naye afisa wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa na naibu wa OCHA nchini Ivory Coast Carlos Geha amesema hali ni ya wasiwasi na watu zaidi ya milioni moja wamekimbia.

(SAUTI YA CARLOS GEHA)