Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya juhudi mabomu ya kutegwa ardhini bado yanakatili maisha ya watu

Licha ya juhudi mabomu ya kutegwa ardhini bado yanakatili maisha ya watu

Licha ya hatua za kupiga marufuku mabomu ya kutegwa ardhini, silaha hizi zinaendelea kuuwa watu hasa katika nchi zinazoendelea ambazo hazina uwezo wa kutoa mabomu hayo.

Aprili 4 kila mwaka inaadhimishwa siku ya kimataifa ya kuelimisha na kusaidia mpango wa hatua dhidi ya mabomu hayo na kuifanya dunia kujikita katika tatizo hilo ambalo pia linaathiri pakubwa maisha ya watu.

Katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema maelfu ya watu wanapata elimu kutoka Umoja wa Mataifa ya jinsi ya kuzuia hatari ya kuuawa kwa mabomu ya ardhini.

Nchini Afghanistan pekee watu 14,400 wamameajiriwa kuharibu zaidi ya mabaki milioni moja ya mabomu ya vita. Hata hivyo licha ya mafanikio kiasi juhudi bado zinahitajika kama anavyosema Takuto Kubo kutoka mpango wa Umoja wa Mataifa wa hatua dhidi ya mabomu ya ardhini.

(SAUTI YA TAKUTO KUBO)