Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mauaji ya wafanyakazi wake Afghanistan:Ban

UM walaani mauaji ya wafanyakazi wake Afghanistan:Ban

Wafanyakazi takriban wanane wa Umoja wa Mataifa wameuawa nchini Afghanistan hii leo na wengine kujeruhiwa baada ya waandamanaji kushambulia ofisi za Umoja wa Mataifa katika mji wa Mazar-i-Sharif Kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa shambulio hilo limetokea katika ofisi za mpango wa Umoja wa Mataifa wa msaada kwa Afghanistan UNAMA.

Staffan de Mistura mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa na mkuu wa UNAMA nchini Afghanistan anaelekea mjini Mazar-i-Sharif kukabiliana na hali iliyotokea.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliyeko safari nchini Kenya amelaani vikali shambulio hilo na kusema ni ukatili wa kiuoga na kitendo kisichokubalika.