UNHCR yaitaka Austria kurekebisha sheria za uhamiaji

1 Aprili 2011

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea hofu yake kufuatia mabadiliko yaliyofanyiwa sheria za uhamiaji nchini Austria zinazowanyima haki wahamiaji likisema kuwa iwapo zitatekelezwa zitakuwa na athari hususan kwa watoto.

Mswada wa sheria hiyo unatarajiwa kujadiliwa bungeni juma lijalo na kuanza kutekelezwa baadaye mwezi huu. Baadhi ya sheria hizo zinawalazimu wahamiaji kusalia kwenye vituo vinavyowapokea kwa siku saba huku yule ambaye atakiuka sheria akikabiliwa na adhabu ya kifungo.

UNHCR inasema kuwa sheria hiyo itawanyima wahamiaji haki ya kupata ushauri au kusaidiwa na kuongeza kuwa huenda pia sheria hii ikasababisha kutengana kwa familia kwa muda.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud