UM watupilia mbali kesi ya Georgia mahakama ya ICJ

1 Aprili 2011

Mahakama yenye mamlaka zaidi kwenye Umoja wa Mataifa ICJ umetupilia mbali kesi iliyowasilishwa mbele yake na George ikiishtaki urusi na makundi mengine ya waasi kwa kuendesha mauaji ya kikabila kwa raia wake.

Mahakama hiyo ya ICJ iliyo Hague inasema kuwa haitashughulikia kesi hiyo kwa kuwa majadiliano ya kutafuta suluhu hayakuwa yamefanyika kati ya pande husika. Georgia ilidai kuwa Urusi na waasi hao waliendesha ghasia za kikabila dhidi ya raia wa Georgia kwenye maeneo ya Abkhazia na Ossetia kusini.

Urusi ilichukua udhibiti wa maeneo hayo mawili mwaka 2008 na kusababisha maelfu ya raia wa Georgia kuyakimbia maeneo hayo na ambao hadi sasa ni wakimbizi wa ndani nchini Georgia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud