Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi wa UM wauawa Afghanistan Ban alaani vikali

Wafanyakazi wa UM wauawa Afghanistan Ban alaani vikali

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan wameuawa hii leo baada ya waandamanaji kushambulia ofisi za Umoja wa Mataifa katika mji wa Mazar-i-Sharif Kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa shambulio hilo limetokea katika ofisi za mpango wa Umoja wa Mataifa wa msaada kwa Afghanistan UNAMA. Idadi kamili ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliokufa haijajulikani na UNAMA inasema inajitahidi kupata taarifa kamili na kuwasaidia wafanyakazi walioathirika.

Staffan de Mistura mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa UNAMA nchini Afghanistan anaelekea mjini Mazar-i-Sharif kukabiliana na hali iliyotokea. Tutawapasha taarifa zaidi jinsi zinavyotufikia.