Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wimbi la wakimbizi wa Ivory Coast waingia Ghana:UNHCR

Wimbi la wakimbizi wa Ivory Coast waingia Ghana:UNHCR

Wakimbizi zaidi wanaendelea kukimbilia taifa la Ghana wakati mapigano yakizidi kupamba moto nchini Ivory Coast.

Wakimbizi 130,000 wameripotiwa kuingia nchini Ghana juma hili baada ya kukimbia mapigano kwenye maeneo ya Duekoue, Daloa na Bondoukou. Hadi sasa wakimbizi kutoka Ivory Coast wamekuwa wakitoka mji wa Abidjan ambapo mapigano yaliyoshuhudiwa juma hili yakisababisha watu zaidi kuvuka mapaka.

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limetuma kundi la kuchunguza kiwango cha usaidi wanachohitaji wakimbizi hao. George Njogopa anaarifu.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)