Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kituo cha kukabiliana na uharamia chafunguliwa:UM

Kituo cha kukabiliana na uharamia chafunguliwa:UM

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya ubaharia IMO amezindua kituo cha kwanza mjini Mombasa Kenya kati ya vitatu vya kushirikiana taarifa za kusaidia kupambana na uharamiakwenye bahari ya Hindi na pwani ya Aden.

Kituo hicho mjini Mombasa kilichofunguliwa na katibu mkuu wa IMO Efthimion E. Mitropoulos itatumika kwa pamoja na kituo cha kanda cha ubaharia MRCC ambacho kinafanya kazi saa 24 kupiga doria katika maeneo ya magharibi mwa bahari ya Hindi.

Vituo hivyo vimenzishwa chini ya mkataba wa Djibouti wa kukabiliana na uharamia na unya'nganyi wa kutumia silaha dhidi ya meli Magharibi mwa Bahari ya Hindi na ghuba ya Aden. Mwandishi wa habari Josephat Kioko alikuwepoe kwenye uzinduzi wa kituo hicho na kuandaa taarifa hii.