Pande zote Ivory Coast lazima ziwalinde raia:Ban

Pande zote Ivory Coast lazima ziwalinde raia:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ambaye anafuatilia kwa karibu hali ya Ivory Coast amesema anahofia machafuko yalivyoshika kasi nchini humo.

Amezitaka pande zote kutekeleza wajibu wao wa kukwepa kuwadhuru raia , na kuongeza kwamba ni muhimu kwa pande zote kushirikiana na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast UNOCI katika jukumu la kuwalinda raia.

Ban amerejea kauali yake kwamba wote wanaohusika na kuchochea, kuahasiha au kukiuka haki za binadamu watawajibishwa chini ya sherika za kimataifa.

Pia anatiwa shaka na hali ya kibinadamu katika taifa hilo na nchi jirani ya Liberia na amezitaka pande zote kuruhusu mashirika ya misaada kuwasaidia maelfu ya watu, huku akiitolea wito jumuiya ya kimataifa kuchagia pakubwa ili matatizo ya Ivory Coast yatatuliwe.

Kauli ya Ban imekuja wakati majeshi yanayomuunga mkono Rasi anayetambulika kimataifa Alassane Ouattara yanadhibiti miji kadhaa ya magharibi, kati na mashariki mwa nchi hiyo ukiwepo mji mkuu Yamasoukrou na sasa wanadaiwa kuelekea Abijan.

Kwa mujibu wa UNOCI mkuu wa majeshi ya serikali ya Laurent Gbagbo ameripotiwa kuomba hifadhi kwa balozi wa afrika ya Kusini nchini Ivory Coast.