Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biachara ya bidhaa zilizovumbuliwa itasaidia maendeleo:UM

Biachara ya bidhaa zilizovumbuliwa itasaidia maendeleo:UM

Bishara ya bidhaa na huduma zinazovumbuliwa vimetajwa kama moja ya njia ya kuinua uchumi hususan kwenye nchi zinazoendelea.

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa ni kuwa biashara ya bidhaa zilizovumbuliwa iliendelea kuimarika kila mwaka kwa asilimia 14 hata baada ya ulimwengu kushuhudia hali mbaya ya uchumi.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York pia inasema kuwa biashara ya bidhaa na huduma zilizo vumbuliwa kama vile filamu, muziki, vyombo vipya vya habari, sana na kazi za mkono pamoja na vitabu iliongezeka mara dufu kutoka mwaka 2002 na mwaka 2008 hadi kufikia dola bilioni 600.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa ikiwa biashara hiyo itatunzwa vizuri na kushirikishwa kwenye sekta za kitamaduni inaweza kuchangia kwenye upatikanaji wa ajira na ukuaji wa uchumi.