Mabadiliko ya hali ya hewa kuathiri uzalishaji wa chakula:FAO

31 Machi 2011

Shirika la chakula na kilimo FAO leo limeonya kwamba kuna uwezekano wa athari kubwa za mabadiliko ya hali ya hewa kukumba uzalishaji wa chakula.

FAO ikiwasilisha taarifa yake kwenye kitengo cha mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa cha Umoja wa Mataifa imesema mabadiliko hayo yatazikumba nchi zinazoendelea katika siku za usoni na hatua zinahitajika ili kuwaandaa watakaokumbwa na athari hizo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi msaidizi wa FAO kuhusu rasilimali Alexander Muller hivi sasa dunia imejikita zaidi kutafuta suluhu ya muda mfupi ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa ambazo zimesababishwa na majira tofauti mabaya. Ameongeza kuwa sasa dunia inapaswa pia kujikita katika suluhu ya muda mrefu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter