Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mionzi ya nyuklia Fukushima bado inawatia hofu Wajapan

Mionzi ya nyuklia Fukushima bado inawatia hofu Wajapan

Mionzi ya nyuklia inayoendelea kuvuja kwenye mtambo wa Fukushima Daiichi nchini Japan umewafanya maelfu ya raia wa nchi hiyo kusalia na wasiwasi wa afya zao.

Mionzi iliyoanza kusambaa baada ya kinu cha nyuklia kuharibiwa na tetemeko na tsunami hapo Machi 11. Mionzi hiyo kwa mujibu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA na serikali ya Japan imebainika kwenye maji na baadhi ya vyakula.

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Tokyo Mari Yamashita anasema hali hiyo imeleta hofu kubwa miongoni mwa watu.

(SAUTI YA MARI YAMASHITA)