Gharama za chakula zaongeza umasikini Asia-Pacific:ESCAP

31 Machi 2011

Gharama kubwa za chakula zimezuia watu milioni 19.4 katika nchi za Asia -Pacific kujikwamua na umasikini mwaka jana imesema ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo.

Ripoti hiyo pia inasema kuendelea kupanda kwa bei za chakula na mafuta kumesababisha watu wengine milioni 42 katika eneo hilo kusalia masikini.

Tathimini ya kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya uchumi na jamii kwa Asia na Pacific ESCAP imeonya kwamba ongezeko hilo la bei ya chakula itaahirisha kufikiwa kwa lengo namba moja la maendeleo ya milenia ambalo ni kupunguza kwa nusu umasikini na hasa katika nchi za Bangladesh, India, Jamhuri ya watu wa Lao na Nepal.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter