Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unyanyapaa bado ni tatizo katika vita dhidi ya HIV

Unyanyapaa bado ni tatizo katika vita dhidi ya HIV

Ripoti hiyo iliyozinduliwa leo iitwayo uniting for universal access inasisitiza uvumilivu sufuri dhidi ya maambukizi ya HIV, ubaguzi na vifo vitokanavyo na ugonjwa huo.

Lakini pia imegusia suala la unyanyapaa kuwa bado ni kikwazo. Rebecca Awiti ni muathirika wa Ukimwi nchini Kenya na pia ni mwanaharakati. Anaeleza alivyokabili suala hilo:

(SAUTI YA REBECCA AWITI)

Ripoti hiyo pia imetoa mzimamo wa kimataifa wa hali ya Ukimwi, hatua zilizopigwa kwa malengo yaliyowekwa, changamoto ambazo bado zipo na mapendekezo yatakayojadiliwa na viongozi wa dunia kwenye mkutano wa baraza kuu kuhusu tathimini ya Ukimwi utakaofanyika kuanzia Juni 8 hadi 10 mwaka huu.