Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali inazidi kuwa mbaya Fukushima Daiichi Japan:IAEA

Hali inazidi kuwa mbaya Fukushima Daiichi Japan:IAEA

Hali katika mtambo wa nyuklia wa Fukushima Daiichi ulioharibiwa na tetemeko na tsunami nchini Japan inaendelea kuwa mbaya.

Hiyo ni tathimini ya mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA Yukiya Amano anayetoa taarifa ya hali inayoendelea karibu kila siku mjini Vienna kwenye makao makuu ya shirika hilo. Wafanyakazi wa mtambo huo amesema wameyaweka maisha yao hatarini kutokana na mionzi ambyo sasa imeathiri maji pia ili kuweza kukarabati kinu hicho cha nyuklia.

(SAUTI YA YUKIYA AMANO)

Bwana Amano anaandaa mkutano wa ngazi ya juu wa usalama wa nyuklia utakao fanyika mjini Vienna kuanzia Juni 20 hadi 24 mwaka huu. Inakadiriwa kwamba watu 10,000 wamefariki dunia kwenye tetemeko na tsunami iliyokumba Japan Machi 11.