Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Itakuwa ni matatizo makubwa serikali ya mpito Somalia ikiongeza muda:Mahiga

Itakuwa ni matatizo makubwa serikali ya mpito Somalia ikiongeza muda:Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga amesema itakuwa kitahanani kikubwa endapo serikali ya mpito Somalia itafanikiwa kuongeza muda kama inavyotumai.

Mahiga amesema taifa hilo ambalo linaghbikwa na vita kwa miongo miwili sasa linahitaji kuzingatia mkataba wa amani wa Djibouti, kukamilisha kipindi cha mpito na kuchagua serikali mpya hapo mwezi Agosti mwaka huu.

Amesema nia ya serikali ya mpito inayoongozwa na Rais Sheikh Sharif ambayo inataka kupunguza muda wa bunge na kujiongezea mwaka mmoja kwa sasa iko kwenye tafrani na bunge na haina uwezo wa kuzidisha muda pasi idhibni ya Bunge.

Akizungumza na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha mara baada ya kurejea kutoka Moghadishu kwa kikao cha dharura na serikali ya mpito Balozi Mahiga anafafanua mgogoro unaoendelea Somalia. Ungana nao

(MAHOJIANO NA BALOZI MAHIGA)