Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nusu ya nchi masikini duniani zinaweza kujikwamua ifikapo 2020:UM

Nusu ya nchi masikini duniani zinaweza kujikwamua ifikapo 2020:UM

Nusu ya mataifa 48 maskini zaidi duniani yanaweza kujikwamua kutoka kwa hali yaliyo sasa kwa muda wa maika kumi ikiwa yatafaidika na misaada ya kimaendeleo, kuondolewa kwa ushuru wa bidhaa yanayouza na pia kwa kuongeza maradufu mazao ya kilimo.

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa ni kuwa tangu kuundwa kwa orodha ya nchi maskini duniani na Umoja wa Mataifa mwaka 1970 orodha hiyo imepungua kutoka nchi 51 hadi nchi 48.

Ripoti hiyo iliyotolewa kabla ya kuandaliuwa kwa mkutano kuhusu nchi maskini zaidi duniani mjini Istabul kati ya tarehe 9 na 13 mwezi Mei mwaka huu itatoa mpango wa miaka kumi ya kuwepo kwa usalama wa chakula , ajira bora na nishati safi.

Ripoti ya watu mashuhuri ya mwaka 2011 inasisitiza nchi hizo zinaweza kujikwamua kutoka kwenye umaskini ikiwa zitachukua hatua zenyewe na kupata uungwaji mkono wa kimataifa.