Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali katika mpaka wa Tunisia na Libya imeimarika:WFP

Hali katika mpaka wa Tunisia na Libya imeimarika:WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema hali katika mpaka baina ya Tunisia na Libya imeimarika zaidi ya ilivyokuwa wiki chache zilizopita .

WFP inasema idadi ya watu wanaosubiri kusafirishwa katika mpaka huo imepungua na inaendelea kupungua wakati juhudi za kuwahamisha pia zikishika kasi. Shirika hilo linasema wiki mbili zilizopita idadi ya watu waliokuwa katika kambi hiyo wakisubiri kusafirishwa ilifika 17,000 kwa siku lakini sasa imepungua na kufikia kati ya 7000 na 9000 kwa siku.

Kwa mujibu wa msemaji wa WFP nchini Tunisia Reem Nada WFP pia inaendelea kugawa chakula kwa watu hao.

(SAUTI YA REEM NADA)