Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya wahamiaji kutoka Libya wawasili Italia:UNHCR

Maelfu ya wahamiaji kutoka Libya wawasili Italia:UNHCR

Katika kipindi cha siku nne zilizopita boti za kwanza zimewasili na kuingia moja kwa moja barani Ulaya zikitokea Libya tangu vita vizuke nchini humo.

Zaidi ya watu alfu 2 wasiokuwa wa Libya walikimbia Tripoli kwa kutumia boti kuingia nchini Italy na Malta na hivo kuhitajika sehemu kubwa za mapokezi kwa watu wanaohitaji hifadhi. Boti tano ziliwasili nchini Italy tangu jumamosi jioni zikiwasheheni watu 1484.

Boti mbili ziliwasili Malta jana zikiwa na abiria 535. Wengi kati ya hao ni Wa Eritrea na wasomali wakiwepo akinamama na watoto kati yao. Vilevile wapo wa Ehtiopia,wasudan na idadi kadhaa ya raia wengine. Hadi sasa hakuna walibya walioonekana miongoni mwa hao waliowasili barani Ulaya.

Abiria wa kwanza waliwasili katika kisiwa cha Linosa umbali wa kilomita 50 kaskazini mashariki mwa Lampedusa.Boti zingine mbili ziliwasili nchini Italy siku ya ijumapili,walifikia pia katika kisiwa kidogo cha Linosa kabla ya kupelekwa kwa meli Sicilia. Awali ni boti mbili ziliwasili Sicilia na Lampedusa.

Mama mmoja alijifungua baharini wakati akisubiria huduma huku wengine wawili wakiporomosha mimba haijulikani baharini au baada ya kuwasili ardhini. Wote hao wanaowasili wamekuwa wanalala nje kabla ya kuwahamishia katika vituo vya mapokezi vya Sicilia.

Tawi la umoja wa mataifa la wakimbizi UN HCR limekuwa linazungumza na wakuu wa nchi za Italy na Malta pamoja na shirika la msalaba mwekundu, maana dalili zaonyesha kwamba bado kutakuwa na wimbi kubwa la watu wanakimbia kutoka Libya. Tayari kisiwa cha Lampedusa kimizidiwa na Uwezo wa mapokezi baada ya kuwasili awali maelfu ya wahamiaji kutoka Tunisia wiki kadhaa zilizopita.

Tangu mwezi January ,wakimbizi 19 Elfu wengi wao vijana waliwasili Lampedusa. Wakati huo huo wahamiaji 13 Elfu walihamishiwa katika vituo vya mapokezi vya Sicilia.Zaidi ya wahamiaji elfu sita kutoka Tunisia wamesalia Lampedusa ,idadi kubwa kuliko hata wananchi wa kisiwa hicho wanaokisiwa kuwa Elfu tano.