Mkurugenzo mkuu wa WFP kuzuru nchini Kenya

29 Machi 2011

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kwenda nchini Kenya Afrika ya Mashariki wiki hii.

Afisa huyo ambaye ni mkurugenzi mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Josette Sheeran atafanya ziara ya siku tano nchini Kenya ambapo atahudhuria mikutano muhimu ya Umoja wa Mataifa .

Pia Bi Sheeran atatembelea kambi tatu za wakimbizi za Daadab kaskazini mashariki mwa Kenya zilizo makao kwa wakimbizi 320,000 kutoka Somali. Ramadhani Kibuga na ripoti kamili.

(RIPOTI YA RAMADHAN KIBUGA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter