Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kufanya kongamano la amani baina ya jamii za Kenya na Sudan

IOM kufanya kongamano la amani baina ya jamii za Kenya na Sudan

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na serikali ya Kenya wamendaa kongamano la amani lililo na lengo la kuboresha uhusiano kati ya jamii ya Turkana nchini Kenya na Tuposa nchini Sudan.

Kongamano hilo linafuatia mizozo inayotokana na kunga'nga'nia bidhaa muhimu wakati eneo la kaskazini mwa Kenya likiendelea kukumbwa na ukame.

Kongamano hilo linalotarajiwa kuandaliwa kati ya tarehe 30-31 mwezi huu katika eneo la Lokichoggio nchini Kenya ni sehemu mpango wa unaofadhiliwa na serikali ya Japan kupitia kwa shirika la IOM unaolenga kupunguza mizozo kati ya jamii za wavugaji kaskazini mwa Kenya.

Jamii ya Toposa huvuka na kuingia nchini Kenya ikitafuta malisho huku ile ya Turkana ikivuka na kuingia Sudan kutafuta maji. Japhet Kasimu ni msemaji wa IOM.(SAUTI YA JAPHET KASIMBU)