Skip to main content

Serikali ya Somalia kuongeza muda ni kuongeza adha:UM

Serikali ya Somalia kuongeza muda ni kuongeza adha:UM

Serikali ya Somalia inayoungwa mkono bna Umoja wa Mataifa umeongeza muda wake kupokea udhamini kwa mwaka mmoja zaidi hata baada ya kupokea shutuma kutoka kwa wafadhili na mashambulizi inayokabiliana nayo kutoka kwa wanamgambo.

Tangazo hilo linajiri baada ya bunge la Somalia kuongeza muda wa kuhudumu kwa miaka mitatau zaidi mwezi uliopita. Wanamgambo walio na uhusiano la kundi la al-Qaeda wanadhibiti eneo kubwa la nchi lakini hata hivyo serikali inayoungwa mkono na vikosi vya muungano wa afrika na Umoja wa Mataifa vimechukua udhibiti kwenye mji mkuu Mogadishu kutoka kwa wanamgambo wa al-Shabab.

Muda wa kuhudumu wa serikali hiyo inayokubwa na mizozo ya ndani ungekamilika mwezi Agosti mwa huu. Serikali hiyo inasema kuwa itakuwa vigumu kuandaa uchaguzi. Somalia haijakuwa na serikali dhabiti tangu Siad Barre aondolewe madarakani miaka 20 iliyopita.