Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano mapya Ivory Coast, maelfu wakimbia:UNHCR

Mapigano mapya Ivory Coast, maelfu wakimbia:UNHCR

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema kuwa mapigano makali yameripotiwa katika maeneo ya magharibi mwa Ivory Coast na kusababisha kukwama kwa maelfu ya watu waliokimbia makwao.

IOM inasema kuwa mapigano hayo kati ya vikosi vinavyomuunga mkono Alassane Ouatarra na Laurent Gbagbo yamesababisha kukwama kwa zaidi ya 20,000 kwenye mji wa Duékoué ambapo wengi walikuwa wamepata hifadhi bila makao mwala chakula.

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa kumekuwa na mapigano mapya mashariki mwa Ivory Coast karibu na mpaka na Ghana na kusababisha watu zaidi kuhama makwao. Melissa Fleming kutoka UNHCR hata hivyo anasema kuwa haijabainika iwapo mpaka kati ya Ivory Coast na Liberia umefungwa.

(SAUTI YA MELISA FLEMING)