Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utengezaji bidhaa tofauti utainua uchumi wa nchi maskini:ILO

Utengezaji bidhaa tofauti utainua uchumi wa nchi maskini:ILO

Utengezaji wa bidhaa tofauti pasipo kutegemea bidhaa moja tu imetajwa kama suala muhimu katika kuimarisha uchumi wa nchi maskini.

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa ni kuwa ukuaji wa uchumi kwa muda wa miaka kumi iliyopita kwenye nchi maskini umekuwa wa juu lakini usio dhabiti kutokana na uzalishaji wa bidhaa moja badala ya aina nyingi .

Ripoti hiyo ya ILO inasema kuwa mkutano kuhusu ajira bora kwenye nchi maskini duniani umeandaliwa kufanyika kati ya tarehe 9 na 13 mei mwaka huu mjini Istanbul ili kutoa mpango wa miaka kumi wa kuhakikisha kuwepo kwa usalama wa chakula, ajira nzuri na kupunguza athari za majanga miongoni mwa mataifa 48 maskini duniani.