Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya umma muhimu katika kuijenga upya Sierra Leone:UM

Mashirika ya umma muhimu katika kuijenga upya Sierra Leone:UM

Afisa wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa mashirika ya umma kwa ujumla hususan wanawake yana wajibu muhimu katika kulibadilisha taifa la Sierra Leone kutoka kwa taifa lenye mizozo kwenda kwa taifa lililo na maendeleo.

Akiongea na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mkuu wa afisi inayohusika na shughuli za kutafuta amani nchini Sierra Leone Michael von der Schulenburg amesema kuwa taifa hilo la Afrika magharibi lililokabiliwa na vita vya muda mrefu limekuwa sasa lenye demokrasia halisi.

Taifa la Sierra Leone linapanga kufanya uchaguzi mkuu nwaka ujao, uchaguzi ambao utakuwa muhimu kuonyesha hatua ambazo taifa hilo limefanikiwa kupiga. Bwana von der Schulenburg amewataka wanawake zaidi kushiriki kwenye uchaguzi akisema kuwa ingestahili kuwepo kwa asilimia 30 ya wanawake bungeni baada ya uchaguzi huo.