Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMIT yakabidhi majukumu ya polisi kwa serikali Timor-Leste

UNMIT yakabidhi majukumu ya polisi kwa serikali Timor-Leste

Jeshi la polisi la serikali ya TImor PNTL leo limeanza rasmi majukumu kamili ya kuendesha jeshi hilo kufuatiwa kukabidhiwa mamlaka hayo kwenye hafla iliyofanyika mjini Dili.

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMIT umekamilisha ukabidhi wa majukumu hayo kwa jeshi la polisi la serikali miaka mitano baada ya serikali kuuomba UNMIT kushika udhibiti baada ya kuzuka machafuko.

PNTL sasa inaongoza shughuli zote za polisi nchini humo, lakini hii haimanishi kwamba polisi ya Umoja wa Mataifa UNPOL itaondoka nchini humo. Xanana Gusmao waziri mkuu wa Timor-Leste anaiona hatua hii kama mwanzo wa ukurasa mpya wa UNIPOL kuwa mshauri na kusaidia kusimama imara kwa polisi ya nchi hiyo.

(SAUTI YA XANANA GUSMAO)