Masuala ya watoto yashughulikiwe Sudan Kusini:UNICEF

28 Machi 2011

Naibu mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Hilde F. Jonson amekamilisha ziara ya siku nne Sudan Kusini mwishoni mwa wiki ambako ametathimini na kujionea mwenyewe hali halisi na hatua zilizopigwa kwa wanawake na watoto.

Alipowasili Sudan Machi 18 Bi Jonson alizuru Darfur na Abyei kabla ya kuelekea Sudan kusini . Ziara yake imefanyika miezi miwili baada ya kura ya maoni ya kihistoria iliyoamua kuigawa mapande mawili nchi ya Sudan ifikapo julai 9.

Amesema kutokana na aliyoyashuhudia juhudi zaidi zinahitajika ili kuwalinda wanawake na watoto. Ramadhan Kibuga na ripoti kamili.

(SAUTI YA RAMADHAN KIBUGA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud