Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya waomba hifadhi ughaibuni imepungua:UNHCR

Idadi ya waomba hifadhi ughaibuni imepungua:UNHCR

Idadi ya watu wanaoomba hifadhi katika nchi zilizoendelea imepungua kwa kiasi kikubwa kabisa kwa karibu miaka 10 limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Maombi ya hifadhi takribani 358,800 yaliwasilishwa katika nchi zilizoendelea mwaka jana ambayo yamepungua kwa asilimia tano ikilinganishwa na yale ya 2009. Hata hivyo UNHCR inasema takwimu za mwaka 2010 maombi ni karibu nusu ya yale yaliyowasilishwa mwaka 2001 ambayo yalikuwa 620,000.

Kamisha mkuu wa shirika la wakimbizi Antonio Guterres amesema utafiti zaidi unahitajika kutambua sababu hasa ya kupungua kwa maombi hayo. Fatoumata Lejeune Kaba kutoka UNHCR anafafanua kuhusu hali hii.

(SAUTI YA FATOUMATAKABA)

Kwa Ulaya kupungua zaidi kwa maombi hayo kumebainika Ulaya Kusini katika nchi za Malta, Italia na Ugiriki ambapo maombi yamepungua kwa asilimia 33 ikilinganishwa na mwaka 2009. Marekani alikuwa mpokeaji mkubwa wa waomba hifadhi kwa miaka mitano mfululizo ikiwa inachukua mtu mmoja kila katika maombi sita.