Nchi za maziwa makuu wakutana Rwanda kujadili madini na waasi

25 Machi 2011

Wiki hii wajumbe kutoka nchi 11 za ukanda wa maziwa makuu, wadau wa sekta ya madini na makampuni yanayohusika na biashara ya madini wamekuwa wanakutana mjini Kigali -nchini Rwanda kujadili na kuweka taratibu zitakazohakikisha kwamba madini yanayochimbwa katika nchi za maziwa makuu ni salama , unazingatia mazingira na hauhusishi vikundi vya waasi.

Taratibu hizo pia zitasaidia kuondoa lawama za wizi wa madini zilizokuwepo baina ya nchi jirani na pia kuhakikisha waasi hawatumii madini kama silaha ya vita.Mara kadhaa wanaharakati wa kupigania amani, mashirika ya haki za binadamu na Umoja wa mataifa wamekuwa wakitoa wito kuhakikisha madini yahatumiki kama chachu ya umwagaji damu na vita.

Muandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani KIBUGA amezungumza na katibu mtendaji wa kongamano la maziwa makuu Bi Liberata Mulamula aliyekuwa mkutanoni kuhusu yaliyojiri katika mkutano huo . Ungana nao.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter