Jela miaka 10 mwanaharakati Uchina ni hukumu kali:Pillay

25 Machi 2011

Mwanaharakati wa kupigania demokrasia nchini Uchina Liu Xianbin amehukumiwa kwenda jela miaka 10 kwa makosa ya kutaka kuingilia mamlaka ya serikali.

Xianbin alikabiliwa na hatia hiyo baada ya kuandika makala kadhaa zinazotoa wito wa kufanyika mabadiliko ya kidemokrasia nchini China. Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema anahofia kwamba hukumu hiyo ni kali mno kwa sababu kutoa maoni sio uhalifu.

Bi Pillay pia amesema ongezeko la watu kufungwa, vifungo vya nyumbani na vizuizi vingine kwa wanasheria na watetea haki za binadamu nchini Uchina vinatia wasiwasi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter