IOM yaanza kuwasafirisha wahamiaji waliokwamba Benghazi

IOM yaanza kuwasafirisha wahamiaji waliokwamba Benghazi

Shughuli za kuwakoa wahamiaji waliokwama katika bandari ya Benghazi nchini Libya ambao wanasafirishwa hadi katika eneo la Salum lililoko Misri zimerejeshwa upya na tayari shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limesema watu kadhaa wameshaokolewa.

Shughuli hizo zilisimama kwa muda kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama kwenye eneo hilo lakini sasa IOM imeamua kurejelea zoezi hilo ambapo imearifu kuwa watu 146 ambao ni raia wa Chad na wengine 4 kutoka Bangladesh wameshaokolewa.

 

Raia wengine 646 wa Chad wanatazamiwa kusafirishwa hadi mpakani mwa Misri katika kipindi cha siku mbili kuanzia sasa. Hii ni habari njema kwa mamia waliokwama kwenye eneo hilo ambao pamoja na kuhofia hali ya usalama lakini ustawi wa maisha limekuwa jambo adimu kwao.