Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika Magharibu karibu itatokomeza polio:WHO

Afrika Magharibu karibu itatokomeza polio:WHO

Maafisa wa afya wamethibitisha kuwa tatizo la ugonjwa wa Polio kwenye nchin za magharibi mwa Afrika limekaribia kumalizwa.

Tangu mwaka 2009 ugonjwa wa polio umeripotiwa kwenye mataifa 11 magharibi mwa Afrika ambapo ulisababisha vifo vya watu wengi na pia kuwalemaza mamia ya watoto. Chanjo dhidi ya ugonjwa huu zilizo tolewa mwaka 2009 na mwaka 2010 zimefanikiwa kuuangamiza ugonjwa huu.

Pia kampeni nyingine ya kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa huo itakayotolewa mwezi huu na mwezi ujao kwenye nchi 15 itawalenga watoto milioni 38 na kuangamiza dalili zozote za ugonjwa huu ambazo zitakuwa zimesalia. Fadela Chaib ni kutoka WHO.

(SAUTI YA FADELA CHAIB)