Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi waendelea kukimbia machafuko Libya:UM

Watu zaidi waendelea kukimbia machafuko Libya:UM

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa linaendelea kupokea ripoti za watu wanaondelea kuhama makwao mashariki mwa Libya.

Inakadiriwa kuwa hadi watu 20,000 wamekuwa wakipiga kambi kwenye mji mdogo wa Al Butwen kwa zaidi ya wiki mbili huku watu wengine wakihama makwao kwenye mji wa Derna. Hadi sasa UNHCR imetuma makundi mawili na madawa kwenda mji wa Benghazi kupitia kwa shirika la msalaba mwekundu nchini Libya.

UNHCR pia inasema kuwa imetuma mablanketi na misaada mingine. Watu zaidi wanaendelewa kuvuka mpaka wa Libya na kuingia nchini Tunisia hususan wahamiaji kutoka Bangladesh na Sudan.