Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali yazidi kuwa mbaya Ivory Coast:UNHCR

Hali yazidi kuwa mbaya Ivory Coast:UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa maelfu ya watu wanaohofia kutokea kwa vita wanaendelea kukimbia makwao kwenye mji mkuu wa Ivory Coast Abidjan na sehemu zingine za magharibi mwa nchi.

UNHCR pamoja na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM yanasema kuwa karibu watu milioni moja wameukimbia mji wa Abidjan huku watu nusu milioni wakiripotiwa kukimbia makwao magharibi mwa nchi. Melissa Fleming ni kutoka UNHCR na anasema kuwa sasa kuna wakimbizi 100,000 kutoka Ivory waliokimbilia Liberia.

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)

Naye kamishina wa tume ya haki za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa anasema kuwa zaidi ya watu 462 wameuawa tangu kuanza kwa mzozo nchini Ivory Coast mwezi Disemba mwaka uliopita.