Ban Ki-moon atiwa moyo na ari ya vijana Misri

25 Machi 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa ametiwa moyo na jinsi vijana nchini Misri wanavyojaribu kujenga demokrasia mpya kwenye taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.

Hivi majuzi Ban alifanya ziara nchini Misri na Tunisia kufuatia mapinduzi ya raia dhidi ya tawala za kiimla, mapinduzi ambayo yalikuwa yakiongozwa na vijana. Kwenye mahojiano ya kipekee na Radio ya Umoja wa Mataifa Ban alifurahishwa na jinsi maafisa wa ngazi za juu serikali walikuwa na uhuru wa kuongea kwa mara ya kwanza kabisa.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa unatarajiwa kutuma ujumbe kwenda nchini Misri ambapo utakutana na viongozi wa kijeshi nchini humo , makundi ya kutetea haki za binadamu pamoja na wanaharakati.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter