Watu wanpashwa kuelimishwa kuhusu utumwa na biashara ya utumwa:Ban

25 Machi 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa biashara ya utumwa ilisababisha mateso makubwa kwa mamilioni ya watu wasio na hatia kwa muda wa karne nne.

Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka waathiriwa wa biashara ya utumwa Ban amesema kuwa kuiadhimisha siku hii kutasaidia kuzuia dhuluma zozote dhidi ya ubinadamu na kuwarejeshea heshima wanaodhulumiwa.

Ban ametoa wito wa kuangazia vitendo vinavyohusiana na biashara ya utumwa. Huyu hapa Raymond Wolfe mwakilishi wa kudumu kutoka Jamaica kwenye Umoja wa Mataifa ambaye pia amekuwa kwenye msitari wa mbele katika kuadhimisha siku hii.

(SAUTI YA RAYMOND WOLFE)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter