Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Libya inakaidi azimio la baraza la usalama:Ban

Serikali ya Libya inakaidi azimio la baraza la usalama:Ban

Serikali ya Libya haijaacha mashambulizi au kutangaza kusitisha mapigano kama ilivyotakiwa na azimio la baraza la usalama kwa mujibu wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Akitoa taarifa kwenye baraza la usalama hii leo kuhusu hali ya Libya Ban amesema tangu mwanzo wa mgogoro katika taiafa hilo la Afrika ya Kaskazini Umoja wa Mataifa umekuwa ukijihusisha katika juhudi za kidiplomasia za kupata ufumbuzi.

Ban ameliambia baraza hilo amekuwa katika mawasiliano na pande zote husika ikiwemo serikali ya Libya.

Libya imekuwa ikirejea kusema imesitisha mapigano, ikiwa ni pamoja na kwa njia ya simu niliyopigiwa na waziri mkuu Machi 19. Hatuoni ushahidi wowote kwamba hivyo ndivyo ilivyo. Nchini humo bado kuna mapambano makali yanaendelea katika miji ya Ajdabiya, Misratah na zitani .