Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uingereza na Australia yaipa IOM zaidi ya dola milioni 6 kwa ajili ya kuendelea kusafirisha wahamiaji

Uingereza na Australia yaipa IOM zaidi ya dola milioni 6 kwa ajili ya kuendelea kusafirisha wahamiaji

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema linaendelea na shughuli ya kuwasafirisha maelfu wa wahamiaji wanaokimbia machafuko Libya baada ya kupata msaada wa fedha.

Wiki iliyopita IOM ilielezea hofu ya huenda ikasitisha zoezi hilo endapo haitopata msaada wa fedha kufadhili shughuli nzima.

Kwa mujibu wa afisa mawasiliano na habari wa shirika hilo Jumbe Omar Jumbe shirika la Uingereza la msaada wa maendeleo kwa nchi za kigeni limewapa kiasi cha pauni milioni 4 Jumamosi iliyopita na pia dola milioni mbili wamepokea kutoka serikali ya Australia msaada ambao utawasaidia sana kuendelea na zoezi hilo.

Jumbe pia akizungumza na Alice Kariuki wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa ameelezea hali znina ya kusafirisha wahamiaji inavyoendelea.

(MAHOJIANO NA JUMBE OMAR JUMBE)