Zaidi ya 460 wafariki dunia Ivory Coast kutokana na mchafuko:UM

Zaidi ya 460 wafariki dunia Ivory Coast kutokana na mchafuko:UM

Zaidi ya watu 460 wamekufa nchini Ivory Coast tangu mwezi Desemba mwaka jana kufuatia utata uliozuka kwenye uchaguzi mkuu wa Rais katika taifa hilo la Afrika ya Magharibi.

Ghasia zinaongezeka nchini humo wakati Rais Laurent Gbagbo akishikilia msimamo wa kugoma kumruhusu Rais Alassane Ouattara kushika hatamu kama Rais aliyechaguliwa wa Ivory Coast. Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNOCI umezikumbusha pande zote zinazohusika katika machafuko kwamba kushambulia raia kunaweza kuwa ni uahlifu dhidi ya ubinadamu.

UNOCI imeongeza kuwa idadi kubwa ya raia wanaendelea kuukimbia mji wa Abobo, Williamsville na Uboka pia maeneo mengine ambayo ni viunga vya mji mkuu Abijan, kutokana na ukosefu wa chakula na madawa.