Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada unahitajika kwa ajili ya Japan:Michael Douglas

Msaada unahitajika kwa ajili ya Japan:Michael Douglas

Mcheza filamu mashuhuri na mjumbe maalumu wa amani wa Umoja wa Mataifa Michael Douglas amesema dunia inahitaji kuendelea kuisaidia Japan hasa wakati huu.

Douglas akizungumza kwenye studio za Radio ya Umoja wa Mataifa hapa New York hii leo ameelezea juhudi zake za kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi na tsunami lililoikumba Japan Machi 11. Amesema dunia inahitaji kuongeza msaada kwa watu hao.

(SAUTI YA MICHAEL DOUGLAS)

Nadhani wengi wetu tumekuwa na hofu kuhusu msaada wa kimataifa wa fedha, inatia shaka ukilinganisha na kilichotokea Haiti na Katrina, matokeo yake watu wanaamini Japan ambayo hadi hivi karibuni ni ya pili duniani kwa pato la taifa ilikuwa inajitosheleza kiuchumi kukabili hali.

Idara ya polisi nchini Japan inasema zaidi ya watu 9800 wamekufa na wengine 17,500 bado hawajulikani walipo kufuatia tetemeko la tsunami ya mwezi huu.